1.HEWA NA MWANGA:
Hewa ni muhimu kwa kila kiumbe, hivyo banda la kuku ni lazima
liingize hewa safi na kutoa ile chafu na liweze kuingiza mwanga wa kutosha.
1. Kwa kifupi ni kwamba madirisha ya banda ni lazima yawe makubwa
na ya kutosha ili yaingize hewa safi na kutoa ile chafu.
2. Ni vema madirisha haya yawe juu kiasi cha meta moja (1) kutoka
chini ili hewa ipite juu ya vichwa vya kuku.
3. Hewa safi siyo upepo, hivyo jaribu kuzuia upepo mkali kuingia
ndani ya banda la kuku ama sivyo kuku wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na
vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa baridi.
4. Jenga Banda lako kwa kukinga upepo unakotokea na kupanda miti
kuzunguka banda hilo la kuku ili kupunguza kasi ya upepo na kuweka kivuli dhidi
ya jua kali na joto.
2.UKAVU NA USAFI WA NDANI:
Kwa vile kuku si ndege wa majini kama bata , ni jambo la busara
kuhakikisha kuwa mahali anapoishi hapana unyevunyevu.
1. Banda la kuku lijengwe
mahali palipoinuka ili kuzuia maji ya mvua yasiingie.
2. Wajengee kuku uchaga wa kulalia kwa kuweka viguzo vyenye urefu
wa meta moja na kutandika miti juu yake ili usiku walale hapo, kuliko kuwalaza
ardhini au sakafuni.
3. Ukavu wa banda ni muhimu sana hasa kwa vifaranga na kuku
wanaotaga. Ndani ya banda lenye unyevu mayai kuchafuka sana hata wakati
mwingine huoza kwa urahisi na jitihada zako zitakuwa ni bure.
4. Sakafu ya banda ni vizuri ikawa ya zege lakini kutokana na
uhaba wa fedha sakafu inaweza kutengenezwa kwa mabanzi (mabanda yaliyoinuliwa)
au udongo mgumu na au mchanga ambao utafunikwa kwa mabaki ya taka za mpunga na
yale ya mbao.
5. Ili kuepuka unyevunyevu ni vyema eneo/mahali pla kujenga banda
pawe pameinuka na penye kupitisha hewa ya kutosha.
3.PAA LA BANDA:
Paa la banda liwe madhubuti ili kuzuia maji ya mvua kuingia hasa
wakati wa masika. Sakafu ya banda iwe juu zaidi ya usawa wa nje. Paa linaweza
kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati , madebe na kama ikishindikana tumia
nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba katika eneo hilo.
4.MATANDIKO
Nilazima kuweka matandio katika sakafu ya banda la kuku. Sehemu
ambayo kukuwakubwa wanaweza kutagia. Ni vizuri kutumia maranda, na si Pumba
zinazo tokana na mbao
Kuku wanaweza kula pumba za mbao. Kwa kuku wanaohatamia, vipande
vidogo na vilaini vya miti na makapi kama vile pumba za mpunga zinaweza
kutumika
5.NAFASI YA KUFANYA KAZI:
Banda la kuku lisiwe na nguzo au mbao nyingi sana ndani kiasi cha
kumfanya mhudumiaji wa kuku ashindwe kufanya kazi zake. Hali hiyo itamfanya
apoteze muda mwingi katika kuzizunguka nguzo hizo, hasa wakati wa kuokota mayai
au kufanya usafi.
6.VIFAA:
Unapotaka kujenga banda la kuku kwanza kabisa tayarisha vifaa
vinavyotakiwa. Vitu kama miti au nyasi, nyavu au fito, misumari au kamba ni
muhimu kuviandaa mapema.
Pili ni lazima uwe na plani/ramani kamili ya banda hilo. Kwa
wastani kila kuku anahitaji nafasi ya Meta za eneo la 0.11 hadi 0.22 (futi 1
hadi 2 za eneo.) kutegemeana na umri wa kuku.
7.UJENZI RAHISI:
Kuku wafugwao hatimaye ni lazima wafidie gharama za Ujenzi wa
mabanda na chakula. Gharama zikiwa kubwa sana huenda ukaifanya shughuli ya
ufugaji isiwe na faida hata kidogo hali hiyo itamfanya mfugaji aone ufugaji
hauna maana yoyote kwake. Lakini ukijenga banda lako kwa kutumia vifaa
vinavyopatikana kwa urahisi utaongeza faida zaidi kwakuwa umepunguza gharama za
uendeshaji wa mradi.
8.VIPIMO:
Banda la kuku linatakiwa liwe na Meta 15 hadi meta 22 za eneo
yaani Meta 3 hadi 4.5 za upana kwa meta 5 za urefu. Banda hili linaweza kutunza
kuku 100 wakubwa kwa wakati mmoja.
HITIMISHO:
• Ujenzi wa mabanda unasisitizwa katika kuboresha ufugaji wa kuku
wa asili ili;
• Kuongeza uzalishaji na kupunguza vifo vya vifaranga kwa majanga
mbalimbali kama vicheche, mwewe, mapaka, mbwa na wizi wa kuku wanaozurura
holela.
• Vile vile inatarajiwa kwamba kuku wanaozuiliwa kwenye banda na
kuwekewa chakula mchanganyiko wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.