MABANDA

UBORA KATIKA MABANDA Miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe ni wa asili au wale walioboreshwa ni ujenzi wa mabanda bora . Hata hivyo si kila mtindo wa ujenzi unafaa, kwahiyo ujenzi huo ni lazima uzingatie mahitaji halisi ili ufugaji huo uweze kutoa matokeo bora yanayotarajiwa na mfugaji. kuna mifumo ya kufuga kuku kama ifuatavyo.ufugaji huria,ufugaji wa ndani kwa ndani na ufugaji wa nje kwa ndani. kuku wakiwa huru kuzuzura na kujitaftia chakula tunazungumzia mfumo huru.kiwango cha uwekezaji unakua mdogo na banda mara nyingi sio muhimu. Mfumo wa ndani kwa ndani (Intensive systems),deep litter 4-5birds/m2 slatted or wire-floor system 6-8birds/m2 umeendelezwa kwa matumizi ya jamii maalum za kuku.asilimia kubwa ya ufugaji wa aina hii upo maeneo ya miji penye soko zuri la mayai na nyama.uwekezaji wake ni wa kiwango Zaidi upande wa mtaji na nguvu kazi.mfano mabanda yenye eneo la mazoezi.aina hii ya ufugaji hufuga maelfu ya kuku. Kwenye mfumo wa nje kwa ndani (semi-intensive ) aina hii a ufugaji huchukua idadi ya kuku 50-200.ufundi na utaalamu hutumika kufugia idadi ya kuku itakayotosheleza. . MAMBO YA MUHIMU KATIKA UJENZI WA BANDA LA KUKU Lizuie upepo mkali wakati wa baridi. Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya chakula na maji. Lizuie kuingia wanyama na wadudu hatari kama vile ndege wa porini,nyoka,panya n.k. Liwe la kudumu ila la gharama nafuu . Liwe nafasi ya kutosha ya kula,kunywa, kucheza na kulala. Liwe kavu daima. Liingize hewa safi wakati wote na kutoa harufu kali ya kinyesi au uvundo.
...