Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Showing posts with label MAKALA. Show all posts

LISHE BORA KWA KUKU




“Kwa takriban asilimia 70% za gharama za ufugaji kuku zimefunganana kwenye ununuzi wa chakula, kuna uhitaji mkubwa wa kutafuta viambato vya chakula vya bei nafuu .”


Na Dennis Kamily
Kuku kama walivyo viumbe wengine walio na uhai huhitaji chakula bora kwa ajili ya afya nzuri na pia kutoa nyama na mayai ya kutosha.
Chakula hiki ni kile kilicho na mhanganyiko mzuri wa viini lishe aina ya protin,wanga mafuta,vitamini,madini na maji salama ya kunywa.

WANGA
Vyakula vyenye asili ya wanga katika miili ya kuku huipatia nguvu na pia huongeza joto la mwili. Vyakula hivi hutokana na mazao ya nafaka kama mahindi,mtama,mpunga na ngano.kiasi kitakacho hitajiaka katika utengenezaji hutegemea na kiasi cha chakula na umri wa kundi la kuku wanaotengenezewa.

PROTINI
Hupatikana kutokana na nyama,samaki,dagaa,soya na mashudu ya pamba,alizeti na mengineyo mara nyingi katika kundi hili la protini huwa vimechanganyika na madini ya chuma. kazi kubwa ya kundi hili ni kujenga na kukuza mwili.

MADINI NA VITAMINI
Madini huweza kupatikana kwa kiasi kidogo kwenye vyakula anavyokula kula kuku.Vitamini huhitajika
katika ukuaji wa kuku,huwapatia kuku hamu ya kula,usagaji wa chakula tumboni,pia husaidia katika utagaji na kuangua wa mayai. Vitamini hupatikana kutokana na majani mabchi,nyama,samaki na matunda.

MAFUTA
Vyakula aina ya mafuta huwa vinachanganyikana na hupatikana katika vyakula vya wanga kama pumba
na nafaka.Vile vile nyama,samaki,mashudu ya alizeti,pamba na ufuta.kazi kubwa ya mafuata ni kutia joto mwili

MAJI
Asilima kubwa ya uzito wa kuku ni maji. Maji haya husaidia kusafirisha chakula chakula mwilini.
husaidia pia kurekebisha joto la mwili,hata hivyo sehemu kubwa ya damu ni maji.

Kwa takriban asilimia 70% za gharama za ufugaji kuku zimefunganana kwenye ununuzi wa chakula, kuna uhitaji mkubwa wa kutafuta viambato vya chakula vya bei nafuu,mfano mabaki ya bidhaa vitokanavyo na vyakula vya binadamu pia kutokana na uzalishaji wa bidhaa zisizo na asili ya wanyama vinakaribishwa kufanyiwa utafiti.mabaki ya viwandani yanatoa nguvu na viini lishe lakini yatumike kwa wastani kwenye chakula cha kuku.

 PAKUA PDF
                                                                      

WAJUE KUKU WENYE FAIDA


kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga ili ikuletee faida uliyodhamiria. Ufugaji unaweza kukutengenezea kipato cha ziada au kukupa ajira ya kudumu kama utazingatia yafuatayo.


1. GHARAMA
gharama zitakuongoza kufanya uchaguzi.kuku wa kisasa ni gharama sana.
pia wanahitaji usimamizi wa hali ya juu,lishe kamili na bora ilikuwawezesha kuzalisha
vizuri na kwa ufanisi.kuku wa kienyeji/asili wana gharama ndogo na rahisi kuzoea mazingira ya huku kwetu.
wakipata matunzo bora wanaweza kuboresha uzalishaji.hata hivyo ukitaka kufuga idadi
kubwa na kutumia mlo kamili(balance diet),ni vyema kuchagua kuku chotara(hybrid).

(picha 1.kuku wa asili akilea vifaranga)         



2.HALI HALISI YA SOKO
ni muhimu sana kuzingatia hali halisi au uhitaji wa soko lililokuzunguka.kama soko lipo la kuridhisha
chagua kuku chotara wenye uzito wa wastani.kama mayai na nyama vinatoka na pia upatikanaj wa mlo kamili     (kuku wa kahawia) ni wa uhakika.
kama unataka kuuza mayai,zingatia jamii ya kuku wepesi (light breed) kuku wale weupe wa mayai.
mazingira mengine tofauti na hapo chagua jamii ya kuku wazito(heavier) mara nyingi wale wa kahawia (brown layers)  ndio chaguo linalostahili.
kama unaishi maeneo ya mbali na soko na unataka kuzalisha mayai kwa matumizi ya nyumbani,na kuuza mayai ya ziada
na nyama kwenye eneo ulilopo,hapo chagua kuku wa asili/kienyeji.











(picha 2.mfugaji akilisha kuku wa kisasa brown layers)

 3.UZOEFU
kuna msemo unasema "experience is the best teacher" mwalimu mzuri n uzoefu,kama huna uzoefu hata kidogo ni vyema ukaanza
 kwa kufuga kuku wa asili ambao ni wa gharama nafuu.

4.USIMAMIZI WA MRADI/BANDA
kama usimamizi wa banda au mradi wako ni mzuri,anza kufuga kuku wa kisasa ambao wanafaida kubwa usimamizi mbovu ni sababu mojawapo ya kushindwa kufanya vizuri kwa miradi mingi na hivyo kupelekea kufungwa.usimamizi kwenye :usafi,kulisha kiasi sahihi na kwa muda muafaka,kutoa taarifa haraka,utunzaji kumbukumbu na mengineyo.


5.MAPENDEKEZO YA WENYEJI
inategemea na maeneo,sehemu nyingine hasa mjini,watu hupendelea mayai ya kahawia au yenye kiini cha njano,wengine wanapendelea
mayai ya rangi nyeupe.kumbuka "mteja ni mfalme".

 6.UPATIKANAJI WA MBEGU ZA KUKU KIURAHISI
kuku hawa wa kisasa mara nyingi huwa hawapatikani kwa urahisi,inategemea na upatikanaji katika eneo husika.

(picha ya 3: mitetea weupe wa aina light breed)




...