kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua
aina bora ya kuku wa kufuga ili ikuletee faida uliyodhamiria. Ufugaji unaweza
kukutengenezea kipato cha ziada au kukupa ajira ya kudumu kama utazingatia
yafuatayo.
1.
GHARAMA
gharama zitakuongoza kufanya uchaguzi.kuku wa
kisasa ni gharama sana.
pia wanahitaji usimamizi wa hali ya juu,lishe
kamili na bora ilikuwawezesha kuzalisha
vizuri na kwa ufanisi.kuku wa kienyeji/asili wana
gharama ndogo na rahisi kuzoea mazingira ya huku kwetu.
wakipata matunzo bora wanaweza kuboresha
uzalishaji.hata hivyo ukitaka kufuga idadi
kubwa na kutumia mlo kamili(balance diet),ni vyema
kuchagua kuku chotara(hybrid).
(picha
1.kuku wa asili akilea vifaranga)
2.HALI
HALISI YA SOKO
ni muhimu sana kuzingatia hali halisi au uhitaji
wa soko lililokuzunguka.kama soko lipo la kuridhisha
chagua kuku chotara wenye uzito wa wastani.kama
mayai na nyama vinatoka na pia upatikanaj wa mlo kamili (kuku wa kahawia) ni wa uhakika.
kama unataka kuuza mayai,zingatia jamii ya kuku
wepesi (light breed) kuku wale weupe wa mayai.
kama unaishi maeneo ya mbali na soko na unataka
kuzalisha mayai kwa matumizi ya nyumbani,na kuuza mayai ya ziada
na nyama kwenye eneo ulilopo,hapo chagua kuku wa
asili/kienyeji.
3.UZOEFU
kuna msemo unasema "experience is the best
teacher" mwalimu mzuri n uzoefu,kama huna uzoefu hata kidogo ni vyema
ukaanza
kwa kufuga
kuku wa asili ambao ni wa gharama nafuu.
4.USIMAMIZI
WA MRADI/BANDA
kama usimamizi wa banda au mradi wako ni
mzuri,anza kufuga kuku wa kisasa ambao wanafaida kubwa usimamizi mbovu ni
sababu mojawapo ya kushindwa kufanya vizuri kwa miradi mingi na hivyo kupelekea
kufungwa.usimamizi kwenye :usafi,kulisha kiasi sahihi na kwa muda muafaka,kutoa
taarifa haraka,utunzaji kumbukumbu na mengineyo.
5.MAPENDEKEZO
YA WENYEJI
inategemea na maeneo,sehemu nyingine hasa
mjini,watu hupendelea mayai ya kahawia au yenye kiini cha njano,wengine
wanapendelea
mayai ya rangi nyeupe.kumbuka "mteja ni
mfalme".
6.UPATIKANAJI WA MBEGU ZA KUKU KIURAHISI
kuku hawa wa kisasa mara nyingi huwa hawapatikani
kwa urahisi,inategemea na upatikanaji katika eneo husika.
(picha ya 3: mitetea weupe wa aina light breed)