MINYOO YA KUKU
UTANGULIZI
Minyoo ya kuku ni
hatari kwani huleta hasara kubwa kwa mfugaji wa kuku wa nyama na mayai. Minyoo
husababisha vifo vingi kwa kuku na hivyo kumkosesha kipato na mtaji mfugaji.
Hata hivyo; licha ya madhara lukuki, ni wakulima wachache mno huchukua hatua
mahusisi za kulikabili na kuthibiti tatizo hili.
AINA ZA MINYOO YA KUKU
i.
MINYOO
MVIRINGO
ii.
MINYOO
BAPA
MINYOO MVIRINGO
(a)
Ascaridia galli
-Ni mkubwa kuliko
minyoo mviringo yote ya kuku.
-Hupatikana katika
utumbo
mwembamba wa kuku
-Ipo aina dume ya
minyoo yenye urefu
yapata sm 3 hadi sm 8 na minyoo ya
kike yenye urefu wa sm 6 hadi sm 12.
(b)
Heterakis gallinae
-Hupatikana katika
utumbo mpana.
-Minyoo dume ina
urefu wa mm 4 hadi
mm 13 na ya kike ina urefu wa mm 8
hadi mm15.
(c)
Syngamus trachea
Hupatikana kwenye koo
Minyoo jike ina urefu
wa mm 25 hadi mm 40. Minyoo dume huwa na urefu mm 2 hadi mm 6.
(d)
Oxyspirura mansoni
Hupatikana kwenye
macho (conjuctival sac)
Minyoo jike ina urefu
wa mm 12 hadi mm 19.
(e)
Gongylonema
ingluvicola
Hupatikana
katika umio au gole la
ndege.
Minyoo
jike ina urefu ya pata mm 32
hadi mm
55.
(f) Cheilospirura hamulosa
Hupatikana kwenye
firigisi.
Minyoo jike ina urefu
wa mm 16 hadi mm 25.
(g)
Tetrameres americana
Hupatikana karibu na
firigisi
Minyoo jike huwa na
urefu wa mm 3.5
hadi 4.5
(h)
Dyspharynx nasuta.
Hii pia hupatikana
kwenye firigisi, minyoo hii hukua na kufikia mm 10 kwa ile ya kike.
TEGU WA KUKU
·
Minyoo
hii hupatikana kwenye utumbo mwembamba.
·
Huathiri
kuku na jamii ya ndege.
·
Kuku
hupata aina hii ya minyoo kwa kula wadudu wabebao mayai au viini vya minyoo.
Mfano minyoo ardhi (earthworms), konokono, inzi n.k.
·
Ina
umbo bapa.
(a)
Raillietina tetrogona
Urefu
hadi sm 25
Wanapatikana kwenye
utumbo mwembamba
(b)
Raillietina
echinobothridia
Urefu hadi sm 25
Mahali, utumbo
mwembamba.
(c)
Raillietina
cesticillus
Urefu hadi sm 13
Mahali utumbo
mwembamba
(d)
Davainea proglottina.
Urefu hadi mm 3
Mahali, utumbo
mwembamba
(e)
Amoebotaemia
sphenoides
Urefu hadi mm 4
Mahali, utumbo
mwembamba
(f)
Choanotaenia
infundibulum
Urefu hadi cm 30
1.
UENEZWAJI WA MINYOO
·
Kupitia
chakula
·
Kupitia
ngozi
·
Vilevile
kuku kupata minyoo kwa kula wadudu wabebao mayai au viini vya minyoo kama vile
Inzi, konokono n.k.
2.
DALILI ZA MINYOO
·
Kuku
hukosa hamu ya kula
·
Ukondefu
·
Kushuka
chini kwa utagaji wa mayai
·
Kuku
hunyongea
·
Baadhi
ya minyoo hukaba koo na kumfanya kuku ashindwe kupumua
·
Baadhi
ya minyoo huleta muasho kwenye macho.
·
Minyoo
pia huzuia mpito wa chakula na hivyo kuleta njaa kwa kuku.
·
Minyoo
ikizidi huua kuku
·
Kuku
pia huweza kupatwa na maambukizo ya magonjwa nyemelezi hasa pale minyoo
inapotoboa utumbo na kusababisha vidonda. Bakteria huweza kushambulia sehemu
hizi.
·
Upungufu
wa damu.