COCCODIOSIS
Ugonjwa
huu umekuwa ukirudisha maendeleo ya wafugaji wa kuku wa kisasa na wakienyeji
kwa kusababisha vifo vingi Tanzania na duniani kote.
UGONJWA WA
KUHARISHA DAMU NI NINI?
-
Ugonjwa huu wa kuharisha damu unawapata sana
kuku.
UGONJWA HUU
HUENEZWA VIPI?
Ugonjwa
huu huenea kutoka mnyama mmoja hadi mwingine kwa njia zifuatazo:
-
Kula chakula chenye vimelea hai vya ugonjwa.
-
Binadamu huweza kupeleka ugonjwa toka kwenye
banda lenye ugonjwa hadi banda la kuku wasio wagonjwa kupitia viatu, mikono na
nguo.
-
Pia ugonjwa huweza kuenezwa na wadudu kama
vile mende, panya, ndege na wadudu warukao.
JE, NI ZIPI DALILI ZA UGONJWA HUU?
Dalili
za ugonjwa huu zinaweza kuonekana waziwazi au kwa kujificha .
Dalili hizo ni:
- Kuku
kuharisha kinyesi kilichochanganyika na damu na mara nyingine huharisha
damu tupu.
- Kuku
hudhoofika.
- Hatimaye
huweza kufa.
ATHARI ZA
UGONJWA
- Kudhoofisha
vifaranga na hata kuku wakubwa
- Vifo –
kutokana na kupoteza damu nyingi.
- Kuku
hupunguza utagaji wa mayai.
JINSI YA
KUGUNDUA UGONJWA.
- Fanya
uchunguzi mara kwa mara kwa mifugo yako, mabadiliko yoyote ya kuku
kinyesi.
- Peleka
kuku wako wakafanyiwe uchunguzi kwenye maabara za mifugo ikiwa ni pamoja
na kuku walio kufa ili wafanyiwe uchunguzi wa kina.