LAYERS

MAGONJWA YA KUKU WA MAYAI.


NA.
MAGONJWA
DALILI
CHANJO/TIBA
1.
New Castle Disease (Mdondo).
-   Vifo vingi vya ghafla.
-   Kuharisha.
-   Hutokea wakati wowote baada ya wiki mbili.
Chanjo siku ya 7, rudia siku ya 21 kila baada ya wiki 12.
2.
Gumboro.
-   Vifo vya ghafla
-   Kukunja mabawa chini.
-   Kujikusanya pamoja.
-   Kuharisha kinyesu cheupe.
-   Ugonjwa hutokea kuanzia wiki ya 2 hadi 18.
Chanjo siku ya 10 – 14, rudia siku ya 28 na 42 kwa kuku wa mayai.
3.
Avian Leukosis Complex.
-    Mavecks – humpata kuku kuanzia umri wa wiki tatu, lakini mara nyingi ni wiki ya 12 – 24.
-    Dalili ni kupooza mabawa, kuvimba na kufa.
-    Kuvimba miguu, maini, wengu na figo.
Tibu.
4.
Fowl Typhoid .
-   Vifo vya kuku mmoja mmoja.
Tibu tumia antibiotic
5.
Pollorum.
-   Huuwa zaidi vifaranga wadogo kuanzia siku ya kwanza hadi wiki tatu.
-   Vifaranga hujikusanya karibu na chanzo cha joto na kusinzia na kutoka na uharo mweupe.
Zingatia usafi wa mabanda na tiba.
6.
Paratyphoid.
-   Dalili hazionekani, vifo hutokea wiki ya kwanza vifaranga hudumaa, wachovu na wanaweza kuharisha.
Tibu tumia antibiotic
7.
Colibacilosis.
-   Vifo wiki ya kwanza vitovu havikauki.
-   Hushindwa kupumua.
-   Macho na kichwa kuvimba.
-   Tumbo hujaa maji (Ascitis).
Tibu tumia antibiotic
8.
mafua (Coryza)
-   Kupiga chafya.
-   Kutoa makamasi.
-   Kuvimba uso mara chache na kupata pneumonia.
Tibu tumia salfa/fluban/fluquin
9.
Coccidiosis (kuharihsa damu)
-    Dalili zipo nyingi.
-    Kinyesi kuwa na rangi ya ugoro au damu tupu.
-    Vifaranga kudumaa.
Tibu tumia amprolium
10.
Foul Pox (Ndui).
-   Kwa kuku wa mayai.
Kila kuku atachinjwa sahemu katika mbawa. Endelea kuwapa maji ya vitamin.


...