Tatizo la gambayai laini na jinsi ya kutibu
Zaidi: †fuga kuku kibiashara†
May 6, 2015
Gamba-yai
laini – picha naRahim Mruma na Dennis mroki
MADA
ZIJAYO: utengenezaji wa yai ndani ya
mwili wa kuku,
utitiri miguuni( magamba makubwa )scaly mite in chickens
Matarajio ya mfugaji ni kupata mayai
bora na imara kwa mlaji, lakini wakati mwingine kunatokea hitilafu katika idara
ya utengenezaji wa yai ndani ya mwili wa kuku na hivyo kupelekea ujenzi wa yai
kutokamilika na kuwa na yai lenye gamba laini.
NINI HUSABABISHA TATIZO LA GAMBA-YAI
LAINI?
Kuna sababu tatu zilizokuu. Kubwa
zaidi ni upungufu wa madini ya kalshium.
Kiasi kikubwa cha kashium huhitatika
kutengeneza gamba yai(egg shell). Gamba-yai inayokiasi cha 95-97% ya kalshium
kaboneti. Mtetea anahitajika kuwa na usawa wa madini ya kalshium katika chakula ili kurudishia kilichotumika
kutengeneza yai.gamba-yai laini ni kiashiria kwamba uwiano sio sahihi ,hivyo
fikiria kuongezea kiwango cha kalshiamu kwenye chakula kwa kuongeza madini hayo
ya kiwandani (nunua kwenye maduka ya
mifugo) au kwenye magamba-yai yaliyokwisha tumika. Yapitishe jikoni kwanza na
kasha yavunje vunje.hatua hii husaidia kuku kutoskia ladha ya mayai na kujenga
tabia ya kula mayai pindi yanapotagwa.
Epuka kuweka kiwango cha juu sana
cha madini kalshium, kitapelekea kuku kuacha chakula chake cha kawaida na
kudonoa mayai
Sababu nyingine ni ubabe. Makundi
mengine huwa na tabia ya kudonoana. Wale wanyonge maskini ya Mungu,wasiokuwa na
mtetezi hudhoofika nafsi na mwili pia.Hivyo hupelekea kutaga yai lenye
gamba-yai laini.wakati mwingine kuku inawabidi watatue matatizo yao bila ya
kuingiliwa na binadamu.lakini,taizo hili likiwa sugu ni lazima kuingiliwa kati .
suluhisho mojawapo ni kukata mdomo wale wakorofi au wababe. Pia unaweza
kumwekea kuku bikibiti (beak bit) kijiplastiki
flani hivi kinachowekwa kwenye mdomo wa kuku kuzuia tabia kama vile ya
kudonoana .
Kama kalshium sio pungufu kwenye
chakula au msongo(stress) sio kiini cha tatizo la gamba-yai laini kwenye kuku
wako,hivyo vifuatavyo hupelekea tatizo hilo; vidusia/vidudu( parasites),
magonjwa na uwezo hafifu wa kuzaliwa nao(poor genetic).Uvamizi wa chawa( lice)
and utitiri (mite) humpa kuku usumbufu na msongo kiasi cha kushindwa kutaga
mayai ya kawaida au kutotaga kabisa. Kuwatokomeza hao wahusika kutapelekea
taizo la gamba-yai laini kutoweka
Matatizo ya kiafya na magonjwa kama
vile; kideri/mdondo( Newcastle’s disease) mafua ya ndege(avian flu),maambukizi
ya mfumo wa upumuaji(respiratory infection), Egg Drop
Syndrome, n.k. kwa ujumla magonjwa haya
hayana tiba kamili.labda ugonjwa wenyewe utapotea na muda au unashauriwa
uwachinje waadhirika.watakao ugua kwa mara ya kwanza hawataweza kustahimili kama
waliogua wakapona.
Jambo la mwisho, matatizo ya
kuzaliwa nayo (genetic defects) hupelekea tatizo la gamba laini.mtetea anaweza
kuwa na tatizo la uvimbe sugu au kasoro za uteri(tumbo la uzai) linalopelekea
kushindwa gamba kwenye yai.kuku wa aina hii asitumike kabisa kwa kuzalisha
vifaranga (breeding stock). Wataalamu wengine hupendekeza kuwaondoa kuku wenye tatizo hili la kuzaliwa culling.lakini
kuku wa nyumbani huwa kama pambo zaidi kuliko mfugo na hivyo kumuondoa inakuwa
sio muhimu kivile.
3 comments:
hii nzuri tunawaomba wafugaji wa kuku kuwa mnapitia page yetu poultrycare mtapat mengi kuusu kuku
Dankeschön
Post a Comment