MATANDIKO YA BANDA LA KUKU KUYATIBU NA KUTANDIKA BANDANI



banda na mazingira yanayochangia hali ya hewa nzuri
bandani,isiyovuja matandiko makavu yatakayopelekea
afya nzuri na mbole yenye rutuba na dhamani kwa
mazao
Matandiko yawe makavu muda wote.
Mara nyingi ukavu wa matandiko huwa hautiliwi
maanani wakati wa kuandaa banda la kuku hasa
wanaofugiwa ndani.matandiko bora yanapaswa
kuwa na uwezo wa kufyonza unyevunyevu ili
kuweka mazingira safi na salama
bandani.matanda ya mbao laini ni bora na ndio
yanashauriwa sana kitaalamu.
Kuongezeka au kupungua kwa kiwango cha
unyevu kwenye Maranda huleta matatizo katika
mfumo wa upumuaji.kiwango cha unyevu
kinapaswa kuwa 30-70%.
Matandiko makavu sana (<30%) ,vumbi hujaa
bandani wakati kuku wanatemba tembea na
hivyo hupelekea kuwepo kwa vijidudu hewani na
kuku kuwavuta pamoja na hewa.Matokeo yake
mfumo wa upumuaji na wa chakula wa kuku
hujaa vimelea hatari wa magonjwa.
Upande wa pili unyevu ukizidi 70%
bandani,hupelekea mazingira ya bacteria kukua
na kuzaliana na hivyo kuhatarisha afya ya kuku.
Hata hivyo unyevunyevu bandani hupunguza
sehemu kavu bandani kwa kuku kujipumzisha na
kupata starehe.hii husababishwa na hewa chafu
aina ya ammonia mbayo humpa kuku mafadhaiko
(stress),huunguza ngozi na macho ya kuku na
hivyo kushusha thamani ya nyama ya kuku na pia
hupunguza kinga ya kuku dhidi ya kupambana na
maambukizi mengine.

Ni jinsi gani kiwango cha unyevu huongezeka
bandani?

1. kinyesi na hewa anayopumua kuku
2. matandiko huwa na unyevu
3. boma na vyombo vya maji
a) Kuvuja
b) Vyombo vya maji kuwa chini sana na
presha ya maji Bomba za maji bandani
4. Banda bovu
5. hewa kutoka nje ya banda
6. tundu la hewa lisilofaa bandani
7.kuzidisha idadi ya kuku kupita uwazo wa banda

Namna ya kuyatibu Maranda kabla ya kuyaweka
bandani

 Chagua Maranda ya mbao laini.
 Yaanike kwenye jua kama yamelowa au
yana unyevunyevu.
 Kisha yatandaze ndani ya banda kina cha
chini kiwe sentimita 2.5 hadi 7.5.
 Pulizia dawa (formalin 40% 1:2,V-RID).
 Kisha pumzisha banda kabla ya kuingiza
kuku

No comments:

...