SABABU 4 ZAKUKUFANYA ULE MAYAI
kula yai ni njia rahisi
ya kuboresha afya yako.kiini cha yai huwa na madini ya chuma pamoja na kaLshium na ute wa yai huwa na protini za
kutosha.madini ya chuma yanasaidia kuongeza damu mwilini na kalshium huimarisha
mifupa.kama huna tabia ya kula yai hizi hapa sababu za kwanini ule yai:
1.kupata vitamini
yai moja huwalimejazwa
vitamin ambzo ni muhimu kwa afya yako
kwani hufanya kazi mbalimbali
kama kuvunja chakula kuwa nguvu za mwili(B2)
kuzalisha seli hai
nyekundu za damu(VitaB12)
kuongeza uwezo wa macho
kuona (VitA)
inapambana na
vichochezi vya kuzalisha kansa(VitE)
kusaidia watoto
kukua(Vit A & B2)
2.kusaidia kupunguza uzito
je wajua kama kula yai
kunasaidia kupunguza uzito?najua hii itakuchanganya kwakua wengi tunaamini
mayai huongeza uzito.lakini utafiti uliofanywa na taasisi ya Rochester Center
for Obesity Research imegundua kuwa kula mayai wakati wa asubuhi inaweka ukomo
wa kiwango cha uhitaji wa *kalorie kwa siku,kwa zaidi ya kalori 400.
hii ni kweli kwasababu
mayai yanakufanya ujiskie umeshiba kwa muda mrefu na hivyo inapelekea wewe
kutokula chochote mchana au kati ya asubuhi na mchana.
3.kupata madini muhimu mwilini
mayai huwa yamejazwa
madini chuma,zinki na fosforas ambayo ni muhimu sana kwa afya.wanawake
wanahitaji sana madini ya chuma kwakuwa hupoteza damu nyingi wakati wa siku zao,ikitokea
madini haya yamepungua mara nyingi huwa wanajiskia kuchoka au mwenye harara au
hasira (grumpy).Zinki inasaidia kuimarisha kinga mwili pamoja na kusaidia mwili
kupata virutubisho kutoka kwenye chakula.fosforasi inasaidia afya ya meno na
mifupa.
Na cha ziada ni kwamba
kuna madini yanayopatikana kwa kiasi kidogo (trace elements)kama vile seleniam
na ayodini.ayodini husaidia kutengeneza homoni,na selenium inasaidia kuondoa
uwezekano wa kupata kansa.
4.kupata protini yenye kalori ndogo
yai lenye uzito wa
wastani huwalina kalori 70-85 na gramu 6.5 za protini.mwanamke anahitaji gramu
50.
hivyo mayai matatu
yatatoa gramu 19.5 karibia nusu ya mahitaji ya siku.(kwa uhakika mahitaji ya
protini mwilini hutegemea na uzito na baadhi ya shughuli anazofanya mtu.
*kalori-kizio/kipimo
cha joto litolewalo na chakula