JE, UNAWAFAHAMU KUKU WA MAYAI?


Kuku hawa walizalishwa nchini ufaransa kwenye miaka ya 1978,Neno I.S.A ni kifupi cha maneno ya kifaransa Institute de Selection Animale.
kuku hawa ni matokeo ya kizazi cha aina nyingi za kuku ambazo ni siri ya kampuni mama iliyowazalisha na yenye haki miliki kisheria.
🐔MAUMBILE
kwa muonekano ni kuku wa wastani sio wakubwa sana,maumbo yao ya mstatili upande wa nyuma ukiwaumejaa zaidi.mikia yao huwa nakuwa juu.
wana upanga mmoja ulionyookea juu.macho yao yanarangi njano na wengine kama naelekea nyekundu na wanafikia hadi kilo 2.2
UZALIANAJI
Kutokana na namna walivyozalishwa ukitotolesha mayai waliotaga huwezi kupata kifaranga mwenye uwezo kama wa wazazi wao.
Mbali na uwezo wao kuwa mdogo bado pia wanachangamoto ya kuugua hasa magonjwa ya figo ukilinganisha na wazazi wao.
kuku hawa wanavyozalishwa vifaranga-majogoo huwa na rangi nyeupe na vifaranga mitetea na rangi nyekundu
🐔UPOLE
ISA-Brown ni rafiki,na wapole na huwa kimya isipokuwa wakati wa kutetea au wakiwa na njaa.
wakati mwingine wanaweza hata kukurukia bila ya wewe kujua na akakukalia ili apate upendo kutoka kwako.
ni kuku unaoweza kuwafugia kwenye kizimba na wakaendelea na shughui yao ya utagaji lakini pia unaweza kuwaachia nje wakajitaftie wadudu na kudonoa donoa majani.
🐔UTAGAJI
Hawa kina dada💅 wanauwezo wa kutaga zaidi ya mayai 300 kwa mwaka! bila hata likizo ya kupukutisha manyoya na ikitokea wanaanza kutaga mayai haraka iwezekanavyo na hii kuwafanya wadada hawa wawe KUKU BORA WA MAYAI.
Kwasababu wanafanya kazi kwa bidii na hivyo kutumia kiwango kikubwa cha viini lishe vya protini na madini ya kalshium kutoka mwilini,inatakiwa wapewe chakula chenye kiwango chajuu kidogo cha protini (+18)-dagaa,damu,soya- na kuongeza madini ya kalshium kupitia DCP,chokaa,mifupa kila wakati hasa kipindi wametoka kupukutisha manyoya.
🐔CHANGAMOTO
hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro ,kuku hawa wanaotaga mwaka mzima wanapozeeka huwa na afya duni na hivyo inashauriwa kuchinjwa na kuwa kitoweo.
mwisho kabisa kuku hawa hawawezi kuhatamia au tuseme inatokea lakini kwa nadra sana.
JE,UNATAKA KUANZA KUFUGA KUKU WENYE AFYA?
Wasiliana nami kwa namba
🤙+255654613488 usipige simu usiku.

No comments:

...