NJIA ZA KUZUIA NYOKA KWENYE BANDA LA KUKU

1.0 ONDOA VISHAWISHI

Kuna baadhia ya vitu ambavyo vinatashawishi nyoka kuliafuata banda la kuku mfano:vifaranga,mayai,panya kumbuka nyoka anapenda kula vitu vidogo vidogo hivyo zuia panya kwa kuondoa chakula bandani au weka mitego

2.0 FANYA USAFI
Ondoa taka taka zinazuzunguka banda au makorokoro yasiyokuwa na kazi ili kuzuia kuwawekea mazingira ya kujificha,pia fyeka nyasi kuzunguka banda.

3.0 ZIBA MIANYA AU MASHIMO
Hakikisha una ziba nyufa uwazi au mashimo kuzunguka banda la kuku hasa mlangoni,kwenye madirisha au nafasi yoyote inayoweza kumwezesha panaya au nyoka kupenya.

4.0 WEKA MITEGO
Kuna namna ya kuweka au kutumia mitego kuzunguka banda kwa nje na ndani ili kuhakikisha anapojaribu kuingia bandani anategwa ,unaweza kuweka yai au hata kifaranga ndani ya mtego ili kumvutia kirahisi.

5.0 TUMIA SUMU AU "repellant"
kuna kemikali au sumu maalum za kufukuza nyoka ila hazipatikani kwa urahisi hivyo njia nyingine zlizoelezwa hapo juu zitumike badala ya.

6.0 TEGA YAI LILILOCHEMSHWA
Ikishindikana kabisa unaweza kuchemshayai la kuku na kisha kuliacha bandani kwani nyoka anapokula mayai husubiri ya pasuke tumboni ndio aondoke hivyo atasubiri mpaka pale utakapomkuta.

No comments:

...