LISHE BORA KWA KUKU




“Kwa takriban asilimia 70% za gharama za ufugaji kuku zimefunganana kwenye ununuzi wa chakula, kuna uhitaji mkubwa wa kutafuta viambato vya chakula vya bei nafuu .”


Na Dennis Kamily
Kuku kama walivyo viumbe wengine walio na uhai huhitaji chakula bora kwa ajili ya afya nzuri na pia kutoa nyama na mayai ya kutosha.
Chakula hiki ni kile kilicho na mhanganyiko mzuri wa viini lishe aina ya protin,wanga mafuta,vitamini,madini na maji salama ya kunywa.

WANGA
Vyakula vyenye asili ya wanga katika miili ya kuku huipatia nguvu na pia huongeza joto la mwili. Vyakula hivi hutokana na mazao ya nafaka kama mahindi,mtama,mpunga na ngano.kiasi kitakacho hitajiaka katika utengenezaji hutegemea na kiasi cha chakula na umri wa kundi la kuku wanaotengenezewa.

PROTINI
Hupatikana kutokana na nyama,samaki,dagaa,soya na mashudu ya pamba,alizeti na mengineyo mara nyingi katika kundi hili la protini huwa vimechanganyika na madini ya chuma. kazi kubwa ya kundi hili ni kujenga na kukuza mwili.

MADINI NA VITAMINI
Madini huweza kupatikana kwa kiasi kidogo kwenye vyakula anavyokula kula kuku.Vitamini huhitajika
katika ukuaji wa kuku,huwapatia kuku hamu ya kula,usagaji wa chakula tumboni,pia husaidia katika utagaji na kuangua wa mayai. Vitamini hupatikana kutokana na majani mabchi,nyama,samaki na matunda.

MAFUTA
Vyakula aina ya mafuta huwa vinachanganyikana na hupatikana katika vyakula vya wanga kama pumba
na nafaka.Vile vile nyama,samaki,mashudu ya alizeti,pamba na ufuta.kazi kubwa ya mafuata ni kutia joto mwili

MAJI
Asilima kubwa ya uzito wa kuku ni maji. Maji haya husaidia kusafirisha chakula chakula mwilini.
husaidia pia kurekebisha joto la mwili,hata hivyo sehemu kubwa ya damu ni maji.

Kwa takriban asilimia 70% za gharama za ufugaji kuku zimefunganana kwenye ununuzi wa chakula, kuna uhitaji mkubwa wa kutafuta viambato vya chakula vya bei nafuu,mfano mabaki ya bidhaa vitokanavyo na vyakula vya binadamu pia kutokana na uzalishaji wa bidhaa zisizo na asili ya wanyama vinakaribishwa kufanyiwa utafiti.mabaki ya viwandani yanatoa nguvu na viini lishe lakini yatumike kwa wastani kwenye chakula cha kuku.

 PAKUA PDF
                                                                      

1 comment:

Unknown said...

Perkenalkan, saya dari tim kumpulbagi. Saya ingin tau, apakah kiranya anda berencana untuk mengoleksi files menggunakan hosting yang baru?
Jika ya, silahkan kunjungi website ini www.kumpulbagi.com untuk info selengkapnya.

Di sana anda bisa dengan bebas share dan mendowload foto-foto keluarga dan trip, music, video, filem dll dalam jumlah dan waktu yang tidak terbatas, setelah registrasi terlebih dahulu. Gratis :)

...