MAHITAJI YA MTAJI WA MRADI
WA KUKU WA NYAMA (200)
1.VIFARANGA
Manunuzi ya vifaranga mia mbili (200) X 1300= Tshs. 260,000/=
2.CHAKULA
MUDA (WIKI) KIASI CHA ULAJI JUMLA
Siku 1 - wiki 1 (siku7) 25g X siku 7 175g
Wiki 1 - wiki 2 (siku7) 50g X siku 7 350g
Wiki 2 - wiki 3 (siku 7) 65g X siku 7 455g
Jumla 980g
Hivyo, kwa kuku wote 200 zitahitajika 980g x kuku 200 = 196000g (196Kg) ambazo ni sawa wastani wa mifuko 4 ya ujazo wa kilogramu 50 kwa gharama ya: = Mifuko 4 x Tshs. 38,000 (bei ya mfuko mmoja)/= =Tshs.152,000/=
Kuanzia wiki ya tatu mpaka ya wiki ya 6 (siku 21), watapewa chakula cha Broiler Finisher kama ifuatavyo:
MUDA (WIKI) KIASI CHA ULAJI JUMLA
Wiki 3 - 4 (siku7) 80g X siku 7 560g
Wiki 4 - 5 (siku7) 110g X siku 7 770g
Wiki 5 - 6 (siku 7) 130g X siku 7 910g
Jumla 2240g
Hivyo kwa kuku wote 200 zitahitajika 2240g x kuku 200 =448,000g (448Kg) sawa na mifuko 9 ya 50Kg,
kwa gharama ya: Mifuko 9 x Tshs 38,000(bei ya mfuko mmoja)/=Tshs. 342,000/=
3.MFANYAKAZI
Wastani wa juu wa gharama za mfanyakazi kwa mwezi ni Tshs. 40,000/=. Hivyo kwa kipindi chote cha ufugaji ni sawa na Tshs. 40,000/= X mwezi 1.5 = Tshs. 60,000
4.MADAWA NA CHANJO
Wastani wa gharama za madawa na chanjo ni Tshs. 50,000/= kwa kipindi chote cha wiki sita kwa kuku wote.
5.BANDA
Kiutaalam, katika eneo la 16m2 wanatakiwa kukaa kuku 200 na gharama za banda/nyumba inakadiriwa kuwa ni Tshs. 5000/= kwa mwezi. Hivyo kwa kipindi chote cha ufugaji (wiki 6/mwezi 1.5) ni sawa na Tshs.5000/= X mwezi 1.5 = Tshs. 7,500/=
4.NISHATI YA MWANGA NA JOTO
Ikiwa gharama za juu za unit moja ya umeme ni Tshs 250/= na zitahitajika balbu 4 kwa muda wa siku 14 za kwanza. Hivyo gharama za umeme ni Tshs. 250 X balbu 4 X siku 14 =Tshs. 14,000/=.
Wastani wa gharama za mkaa kwa siku 14 za mwanzo ni gunia 2 X Tshs. 20,000/=(bei ya gunia moja) ambayo ni sawa na Tshs. 40,000/= kwa kuku wote 200.
5.MAJI
Wastani wa kiasi cha maji kwa kuku wote 200 kwa siku ni ndoo 5 (lita 100), na wastani wa ndoo moja ya maji ni Tshs. 50/=. Hivyo kwa kipindi chote cha ufugaji (wiki 6) ni sawa na Ndoo 5 X wiki 6 (siku42) X Tshs.50/= ni sawa na Tshs. 10,500/= kwa kuku wote 200.
6.MATANDIKO
Wastani wa gharama za matandiko kwa kipindi chote cha ufugaji ni : Tshs.10,000 X mwezi 1.5 = Tsh 15,000/=
7.JUMLA YA MATUMIZI YOTE
Manunuzi ya vifaranga mia mbili (200) Tshs. 260,000/=
Gharama za chakula kwa Broiler Starter Tshs. 152,000/=
Gharama za chakula kwa Broiler Finisher Tshs. 342,000/=
Gharama za mfanyakazi Tshs. 60,000/=
Gharama za madawa na chanjo Tshs. 50,000/=
Gharama za umeme Tshs. 14,000/=
Gharama za maji Tshs. 10,500/=
Gharama za mkaa Tshs. 40,000/=
Gharama za matandiko Tshs. 15,000/=
Gharama za banda/pango Tshs. 7,500/=
JUMLA Tshs. 951,000/=
KUMBUKA: CHANJO NA USAFI NI MUHIMU SANA KWA MATOKEO BORA KWA UFUGAJI WA FAIDA
8. MAPATO YA MAUZO
Wastani wa chini wa mauzo ya kuku ni Tshs.6,500/= (Kila kuku akiwa na uzito wa wastani wa kilo 1.3) kwa kuku, hivyo kwa kuku wote 200 ni sawa na Tshs. 6,500 x kuku 200 = Tshs. 1,300,000/=
Mauzo ya mbolea itakayopatikana yanakadiriwa kuwa Mifuko/viroba 26 na ikiwa wastani wa bei ya kiroba kimoja ni Tshs. 2000/= hivyo jumla ya mauzo ya mbolea ni Mifuko/viroba 26 X Tshs. 3000/ = Tshs. 78,000/=
9.FAIDA
Faida itakayopatikana ni : Tshs. 1,378,000 – Tshs. 951,000 = Tshs. 427,000/= kwa muda wa wiki sita tu, ukitoa gharama zote.
Hivyo, jumla ya mapato yote ni Tshs. 1,378,000/=
MAMBO MUHIMU:
• Matokeo bora ya ufugaji wa faida unaanzia kwenye mazingira/mabanda na sio kwa kuku mwenyewe, hivyo zingatia vipimo vya banda kwa kutambua idadi kamili ya kuku wanaohitajika. (1m2= Broilers 9 – 12)
• Zingatia usafi wa banda kila baada ya kuchafuka au kila baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa.
• Fuatilia ratiba za chanjo bila kukosa kwa kutumia chanjo iliyo salama.
• Ni vyema kufanya matibabu mara tu dalili za ugonjwa zinapoonekana na kuwatenga kuku walioathirika katika kundi.
• Magonjwa karibu yote ya kuku husambaa kwa kinyesi, hivyo epuka mazingira ya kuingiza kinyesi cha kuku mgonjwa bandani kwa kuwa makini kwenye chakula, matandiko, vyombo, n.k.
MAPENDEKEZO
Ni vyema kwa mfugaji kununua chakula kilichotengenezwa kiutaalamu kwa sababu zifuatazo:
a. Kudhibiti magonjwa kwa kuku.
b. Kudhibiti sumu kwa kuku (poisoning i.e mycotixins).
c. Kuepuka uchanganyaji mbaya wa viinilishe kwa kundi husika la kuku.
d. Kuokoa muda na kuongeza jitihada zaidi kwenye uzalishaji.
Hakikisha unakuwa na kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi.
Hakikisha unakuwa karibu na Afisa Mifugo aliye karibu nawe kwa msaada zaidi.
Nunua vifaranga kwenye mashamba yaliyo salama kwa kushirikiana na wataalamu (free from diseases).
Zingatia : Kiwango kizuri cha joto kinachohitajika kwa ufugaji bora wa kuku ambayo ni kati ya 60°F – 90°F (15.6°C – 32 °C).
I POULTRY CARE I
POULTRY CARE itakusaidia mfugaji katika upatikanaji wa soko la uhakika la kuku na ndege wote ufugao(“poultry”).
Wasiliana nasi: