The bird


Mafua ya Kuku (Infectious Coryza )

Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria ambao hushambulia zaidi kuku na ndege wa porini. Ugonjwa
hushambulia kuku wa umri wowote.

Jinsi Ugonjwa Unavyoenea
• Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa.
• Kuku au ndege wagonjwa huambukiza wenzao kupitia mfumo wa hewa wanapopiga chafya.

Dalili
Ugonjwa huu hushambulia zaidi mfumo wa hewa na hivyo kusababisha dalili zifuatazo:
• Makamasi mazito yenye usaha hutoka puani
• Kuku anashindwa kupumua, hukohoa na kupiga chafya
• Harufu mbaya kutoka kinywani na machoni
• Uso mzima unavimba pamoja na upanga
• Vifo vya kuku vinaweza kufikia asilimia 20

Tiba
• Madawa aina ya sulfa na antibiotiki kama vile fluquin/fluban yanaweza kutumika kwa ajili ya tiba na kinga.
...