KUWA MFUGAJI MWENYE MAFANIKIO

Katika kufikia malengo ndio chanzo cha furaha na hasa ndio mafanikio yenyewe.Huwez linganisha mafanikio yako na mtu mwingine kwa kuwa malengo hayafanani.
Watu wengi hawafahamu kuwa kufanikiwa kubiashara ni zaidi ya kuwa na MTAJI, wengi hawafanikiwi kwa kutojiandaa vizuri.
Kufanikio ni kama vita,unajiandaa kwa hali na mali pia kuwa tayari kwa matokeo yoyote,unaposhindwa unatumia fursa hiyo hiyo ili kusimama imara ukifanikiwa unajipongeza, lazima uweke MALENGO na kwa kujitoa muhanga ukifanya hayo utakuwa na uhakika wa kuonja ladha ya mafanikio,kinyume na hapo utaishia kukata tamaa na kuvunjika moyo.
NJIA ZA KUFUATA ILI KUTIMIZA MALENGO YAKO.
#1 andika lengo lako unalokusudia mfano; kufuga kuku wa 5 wa kienyeji wafikie hadi 200
#2 muda au wakati .unatarajia kutimiza ndani ya kipindi cha muda gani?( mfano kipindi cha miezi sita)
#3 hatua utakazofuata. Mfano
Hatua ya 1 andaa banda
2 vifaa,vyombo na vyakula.
3 pata ushauri na msaada wa kitaalam
4 tafuta masoko.
#4 changamoto unazotazamia
Chamgamoto 1 magonjwa
2 masoko
# 5 jinsi ya kupambana na changamoto
# 6 Azimio

.,..........................      .............................
Sahihi                                 tarehe

MSEMO BUSARA
"katika maisha usipiganie kufanikiwa tu,bali pigana kuwa mtu muhimu katika jamii"

Mafanikio mema

No comments:

...