MAHITAJI KUKU WANAOTAGA
Mahitaji ya kuku wanaotaga ni tofauti na makundi mengine.
Mambo ya kuzingatia kwa kuku wanaotaga ni pamoja na:-
• Banda liwe na viota vya kutagia mayai (kiota 1 kwa kuku 3-
5).Viota viwekwe bandani mara kuku watakapofikisha umri wa
wiki 18 ili waanze kuzoea kuvitumia,
• Wapatiwe chakula na maji safi wakati wote kwa kutumia
vyombo maalum ambavyo ni visafi,
• Kuku wasiotaga waondolewe kwenye kundi.Kuku hao
huonekana wasafi na sehemu ya kutolea yai huwa ndogo na
kavu,upanga wake kichwa (comb) huwa mdogo na
mwekundu,
• Wapatiwe dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3,
• Wawekewe fito au ubao mwembamba kama sehemu ya
kupumzikia na mazoezi ili kuzuia kudonoana,
• Mayai yakusanywe mara 4 au zaidi kwa siku ili yasidonolewe
na kuku,
• Kuwe na malalo makavu na yabadilishwe mara yanapochafuka,
• Vyombo vifanyiwe usafi kila ili kuzuia magonjwa; na
• Watundikiwe majani mabichi aina ya mchicha,papai,
alfaafa,majani jamii ya mikunde ili kuboresha lishe.

No comments:

...