MAHITAJI MUHIMU YA BANDA LA KUKU
kuku kama walivyo mifugo wengine wanamahitaji ya muhimu kama vile chakula,mabanda na mambo mengine ila kwa nafasi hii nataka nieleze kidogo kuhusu mahitaji muhimu ya banda la ndege hasa kuku.Yafuatayo ni mambo muhimu katika ujenzi wa banda la kuku
- Nafasi
- Mwanga
- Ulinzi
- Mzunguko Wa Hewa
Nafasi: Idadi Ya Ndege Kulingana Na Eneo Husika
Swala la nafasi ni jambo
muhimu sana katika ujenzi wa banda,kwani nafsi iliyopo itabaini idadi an aina
ya ndege watakaofugwa.kwa mfano,kwa kutumia sakafu yenye Matandiko
(maranda) eneo lenye ukubwa wa mita 6 kwa mita 11 lina uwezo wa kufugia kuku
200 wanaotaga kwa uwiano wa kuku 3 kwenye mita mraba 1
Mbali na hivyo kukun
huhitaji nafasi ya kulala kwenye kichanja. Urefu wa kichanja cha kulalia kwa
kuku hupimwa kwa sentimita.Vipimo vinavyopendekezwa kwa aina 3 za kuku zimeainishwa
kwenye jedwali lifuatalo
JEDWALI 1.0 Mahitaji ya
nafasi ya sakafu na kichanja kwa kuku
AINA YA KUKU
|
NAFSI YA SAKAFU
(kuku/m2)
|
NAFASI YA KICHANJA
(Kwa kuku)
|
mayai
|
3
|
sm 25
|
Chotara(mayai na nyama)
|
4
|
sm 20
|
nyama
|
4-5
|
sm 15-20
|
Kwa uwiano wa kuku 3-4 kwenye nafasi ya mita mraba 1
hufanya makundi ya mitetea kujiskia kuwa huru.kama nafasi Zaidi
itapatikana,tabia nyingi za mitetea zitajidhihirisha. nafasi ikiwa finyu itapelekea
kuku kuwa na tabia zisizo za kawaida,kuwa
dhaifu na kushindwa kukabiliana na magonjwa, kudonoana na kusababisha
waliodhaifu kushindwa kula na kukosa sehemu ya kulala kwenye kichanja.kila kuku
anahitaji nafasi ya kutosha ili kuweza kudhihirisha tabia za kawaida na kuweza
kufanya mazoezi ya kutosha
ikilinganishwa na urundikaji wa kuku kama ilivyo kwa wafugaji wengi.
Matokeo ya nafasi finyu bandani
1 . Uzito mdogo
2 . FC ndogo
3 . Vifo vya
mara kwa mara
4 . Nyama
chache ya kidari
5 . Mlingano
tofauti
6 . Ubora wa
nyama (carcass quality)
No comments:
Post a Comment