Tatizo la gambayai laini na jinsi ya kutibu
Zaidi: †fuga kuku kibiashara†



May 6, 2015
Gamba-yai laini – picha naRahim Mruma na Dennis mroki
MADA ZIJAYO: utengenezaji wa yai ndani ya mwili wa kuku, utitiri miguuni( magamba makubwa )scaly mite in chickens

Matarajio ya mfugaji ni kupata mayai bora na imara kwa mlaji, lakini wakati mwingine kunatokea hitilafu katika idara ya utengenezaji wa yai ndani ya mwili wa kuku na hivyo kupelekea ujenzi wa yai kutokamilika na kuwa na yai lenye gamba laini.

NINI HUSABABISHA TATIZO LA GAMBA-YAI  LAINI?
Kuna sababu tatu zilizokuu. Kubwa zaidi ni upungufu wa madini ya kalshium.  Kiasi kikubwa cha kashium huhitatika kutengeneza gamba yai(egg shell). Gamba-yai inayokiasi cha  95-97% ya kalshium kaboneti. Mtetea anahitajika kuwa na usawa wa madini ya kalshium  katika chakula ili kurudishia kilichotumika kutengeneza yai.gamba-yai laini ni kiashiria kwamba uwiano sio sahihi ,hivyo fikiria kuongezea kiwango cha kalshiamu kwenye chakula kwa kuongeza madini hayo ya kiwandani  (nunua kwenye maduka ya mifugo) au kwenye magamba-yai yaliyokwisha tumika. Yapitishe jikoni kwanza na kasha yavunje vunje.hatua hii husaidia kuku kutoskia ladha ya mayai na kujenga tabia ya kula mayai pindi yanapotagwa.    
Epuka kuweka kiwango cha juu sana cha madini kalshium, kitapelekea kuku kuacha chakula chake cha kawaida na kudonoa  mayai
Sababu nyingine ni ubabe. Makundi mengine huwa na tabia ya kudonoana. Wale wanyonge maskini ya Mungu,wasiokuwa na mtetezi hudhoofika nafsi na mwili pia.Hivyo hupelekea kutaga yai lenye gamba-yai laini.wakati mwingine kuku inawabidi watatue matatizo yao bila ya kuingiliwa na binadamu.lakini,taizo hili likiwa sugu ni lazima kuingiliwa kati . suluhisho mojawapo ni kukata mdomo wale wakorofi au wababe. Pia unaweza kumwekea kuku bikibiti (beak bit) kijiplastiki flani hivi kinachowekwa kwenye mdomo wa kuku kuzuia tabia kama vile ya kudonoana . 
Kama kalshium sio pungufu kwenye chakula au msongo(stress) sio kiini cha tatizo la gamba-yai laini kwenye kuku wako,hivyo vifuatavyo hupelekea tatizo hilo; vidusia/vidudu( parasites), magonjwa na uwezo hafifu wa kuzaliwa nao(poor genetic).Uvamizi wa chawa( lice) and utitiri (mite) humpa kuku usumbufu na msongo kiasi cha kushindwa kutaga mayai ya kawaida au kutotaga kabisa. Kuwatokomeza hao wahusika kutapelekea taizo la gamba-yai laini kutoweka
Matatizo ya kiafya na magonjwa kama vile; kideri/mdondo( Newcastle’s disease) mafua ya ndege(avian flu),maambukizi ya mfumo wa upumuaji(respiratory infection), Egg Drop Syndrome, n.k. kwa ujumla magonjwa haya hayana tiba kamili.labda ugonjwa wenyewe utapotea na muda au unashauriwa uwachinje waadhirika.watakao ugua kwa mara ya kwanza hawataweza kustahimili kama waliogua wakapona.

Jambo la mwisho, matatizo ya kuzaliwa nayo (genetic defects) hupelekea tatizo la gamba laini.mtetea anaweza kuwa na tatizo la uvimbe sugu au kasoro za uteri(tumbo la uzai) linalopelekea kushindwa gamba kwenye yai.kuku wa aina hii asitumike kabisa kwa kuzalisha vifaranga (breeding stock). Wataalamu wengine hupendekeza kuwaondoa  kuku wenye tatizo hili la kuzaliwa culling.lakini kuku wa nyumbani huwa kama pambo zaidi kuliko mfugo na hivyo kumuondoa inakuwa sio muhimu kivile. 

3 comments:

Unknown said...

hii nzuri tunawaomba wafugaji wa kuku kuwa mnapitia page yetu poultrycare mtapat mengi kuusu kuku

Unknown said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

Dankeschön

...