MAHITAJI MUHIMU YA BANDA LA KUKU
   kuku kama walivyo mifugo wengine wanamahitaji ya muhimu kama vile chakula,mabanda na mambo mengine ila kwa nafasi hii nataka nieleze kidogo kuhusu mahitaji muhimu ya banda la ndege hasa kuku.Yafuatayo ni mambo muhimu katika ujenzi wa banda la kuku
  •  Nafasi
  • Mwanga
  • Ulinzi
  • Mzunguko Wa Hewa

Nafasi: Idadi Ya Ndege Kulingana Na Eneo Husika

Swala la nafasi ni jambo muhimu sana katika ujenzi wa banda,kwani nafsi iliyopo itabaini idadi an aina ya ndege watakaofugwa.kwa mfano,kwa kutumia sakafu yenye Matandiko (maranda) eneo lenye ukubwa wa mita 6 kwa mita 11 lina uwezo wa kufugia kuku 200 wanaotaga kwa uwiano wa kuku 3 kwenye mita mraba 1
Mbali na hivyo kukun huhitaji nafasi ya kulala kwenye kichanja. Urefu wa kichanja cha kulalia kwa kuku hupimwa kwa sentimita.Vipimo vinavyopendekezwa kwa aina 3 za kuku zimeainishwa kwenye jedwali lifuatalo

JEDWALI 1.0 Mahitaji ya nafasi ya sakafu na kichanja kwa kuku


AINA YA KUKU

NAFSI YA SAKAFU
(kuku/m2)
NAFASI YA KICHANJA
(Kwa kuku)
 mayai
3
sm 25
Chotara(mayai na nyama)
4
sm 20
nyama
4-5
sm 15-20

Kwa uwiano wa  kuku 3-4 kwenye nafasi ya mita mraba 1 hufanya makundi ya mitetea kujiskia kuwa huru.kama nafasi Zaidi itapatikana,tabia nyingi za mitetea zitajidhihirisha. nafasi ikiwa finyu itapelekea  kuku kuwa na tabia zisizo za kawaida,kuwa dhaifu na kushindwa kukabiliana na magonjwa, kudonoana na kusababisha waliodhaifu kushindwa kula na kukosa sehemu ya kulala kwenye kichanja.kila kuku anahitaji nafasi ya kutosha ili kuweza kudhihirisha tabia za kawaida na kuweza kufanya  mazoezi ya kutosha ikilinganishwa na urundikaji wa kuku kama ilivyo kwa wafugaji wengi.


Matokeo ya nafasi finyu bandani
1                 .     Uzito mdogo
2                 .     FC ndogo
3                 .     Vifo vya mara kwa mara
4                 .     Nyama chache ya kidari
5                 .     Mlingano tofauti
6                 .     Ubora wa nyama (carcass quality)

No comments:

...