KIINI CHA DHAHABU HUTOKANA NA LISHE BORA


Walaji ulimwenguni kote wameanza kutambua umuhimu wa vyakula vyenye afya.wanatambua kuwa kiini cha dhahabu ni alama ya yai safi na salama kutoka kwa kuku mwenye afya.matunzo mazuri,welfare na lishe,pamoja na hayo unaweza kuongeza rangi kwa kutumia virutubisho vya viwandani kama vile carotenoids, hii itasaidia kupata kiini kitakachowavutia walaji duniani kote.
Kiini cha yai hutegemea kiasi cha karotini iliyopo kwenye chakula.Karotini hupatikana kwa njia ya asili kutoka kwenye baadhi ya mimea kama vile lukina lakini pia huandaliwa viwandani kwa njia za kitaalamu n azote hufanya kazi sawa na kubadili rangi ya kiini cha dhahabu.hizi za viwandani pia huwa na rangi ya dhahabu ya kudumu kwenye kiini cha yai kama ilivyo ile ya mimea.mbali na kuwa karotini hufanya yai kuwa na rangi ya kuvutia kwa mlaji lakini pia husaidia yai kutopoteza ubora wake.

No comments:

...