Ugonjwa Sugu wa Mfumo wa Hewa


KWA WAFUGAJI WA BROILER(KUKU WA NYAMA)
NA BATA MZINGA
____________________________________________
Ugonjwa Sugu wa Mfumo wa Hewa
____________________________________________
sababu kuu ya msingi ni bakteria
mara nyingi huchochewa na kideri,
Gumboro hatimaye bakteria huvamia.
sababu zinazopelekea ndege(kuku)
kuugua kirahisi ni wahaka(stress)
unaotokana na kusafirisha/kuhamisha
ndege/kuku,kukata mdomo,baridi,
hewa nzito au uvundo
_____________________________________________
Jinsi Ugonjwa Unavyoenea
Njia kuu ya kuenea kwa maambukizi
ni kupitia mayai, hivyo maambukizi
huendelea kutoka kizazi hadi kizazi.
Pia maambukizi yaawezakuenea kwa kugusana
au kupitia hewa vumbi au ute.
huchukua siku 4-wiki 3 kuonekana siku
ya kuonyesha ugonjwa tayari wanakua
wamekaribia kufa.
_____________________________________________
Jamii ya ndege wanaougua
kuku & bata mzinga
______________________________________________
Dalili
Vifaranga:kupoteza hamu ya kula
kupungua uzito.
kuku au ndege wakubwa:dalili kuu ni kupiga chafya
kukohoa & kushindwa kupumua
wanaotaga:hupunguza kutaga kwa 20-30%
CRD haisababishi vifo vingi na hivyo kupungua kutaga na
kupunguza uzito huonekana mara nyingi,hasa kwa kuku wan-
aotaga.
Kwa hali hii kwa ujumla kubwa hasara hutokea kwa kuku
wa nyama.
___________________________________________________
Uchunguzi wa mzoga
Kamasi nzito zenye usaha zilizotapakaa kwenye pua,
koromeo, mapafu na vifuko vya hewa
utandu wa pafu huwa mzito na mweupe na wenye kamasi
Bata mzinga :huvimba chini ya macho
___________________________________________________
Vipimo vya  maabara
damu,ute,mapafu vya ndege husika hutumika kuchunguza
uwepo wa bakteria
____________________________________________________
Magonjwa yanayofanania
Mzoga wa ugonjwa huu hufanana na kideri,homa ya pafu
maambukizi ya backteria aina ya E.coli
____________________________________________________
TIBA
Madawa aina ya sulfa na antibiotiki kama vile
Tylosin yanaweza kutumika kutibu mayai kutoka kwa waathirika
na vile vile ajili ya kinga na tiba kwa kuku na bata mzinga.
____________________________________________________
Imeandikwa na Dennis Kamily

No comments:

...